Sign Industries Ltd
Sign Industries Ltd
About us

Ukaribisho kutoka kwa mkurugenzi mtendaji

HABARI NA KARIBU KWENYE TOVUTI YETU.

Kusema ukweli, ninapata msisimko mkubwa kukukaribisha hapa kwasababu naamini kabisa unaweza kuona tovuti hii kama namba moja,(#1) na tovuti bora kabisa duniani kuhusiana na Sanaa ya uchoraji kwenye kompyuta (graphics) na alama (vibao na mabango) kuwahi kuiona kwenye mitandao duniani kote. Kwanini ? ni kwasababu tovuti nyingi kwenye mitandao ama hutayarishwa na watu wasio na taaluma au kutengenezewa na mawakala wa makampuni kwa ajili ya biashara tu. Lakini sisi, tumekutengeneza tovuti hii sisi wenyewe kwa minajili ya kukufaa wewe na ili kukupa mwanga na maelezo ya kina, yanayotokana na uzoefu binafsi na rahisi kueleweka.

Maelezo ni rahisi na yapo kwa upana ambayo utakubaliana nayo taratibu kwa kadri unavyoyazamia kuyasoma kwa kina. Wabunifu wetu wa ndani walifanya kazi kwa bidii masaa ishirini nne kuendeleza na kuiweka vizuri hii tovuti kwa kukazia fikra zetu na tulikuwekea jicho letu kwako muda wote.

Kwa miongo minne iliyopita, nilijiingiza kwenye tasnia hii kama mwanafunzi, maneno ya jumla ya kikazi (istilahi) na utaratibu wa kazi wa tasnia hii ilikuwa ikininichanganya na vyote vilikuwa vipya kwangu. Kazi zote zilikuwa za mikono bila mashine, kulikuwa hakuna kompyuta au mashine za CNC na kama mgeni kwenye kazi sehemu kubwa ya kazi zote za kutumia nguvu ya mwili ziliniangukia mimi. Kuchacharika na kujituma kwa muda mrefu kulinikuza kikazi. Ndio nimekomaa katika mazingira hayo, kwa kuwa nilifurahia na kupenda mazingira ya tasnia hii na mtazamo wangu chanya, nimepanda ngazi haraka na hatimaye nikaanzisha biashara yangu inayofanana na hii nikaiita jina la Signs industries Ltd., alama na nembo zake bado zipo vilevile kwa miaka hii yote 22.

Kutokana na msingi wangu mzuri katika tasnia ya Sanaa ya michoro, vielelezo kwenye kompyuta na uchapishaji, na uzoefu wa miaka zaidi ya 40 katika biashara ya mabango ya matangazo na muonekano wa bidhaa kwa wateja, na kwa kuongezea na uzoefu wangu wa maisha binafsi, ilikuwa rahisi sana kwangu kuelewa saikolojia ya mteja na kufahamu jinsi wengine wanavyofikiria hasa wale ambao bado hawajawa na uelewa katika biashara hii ambapo wakati mwingine husita au huona aibu kuuliza maswali mepesi kwa kuogopa kuonekana hawafai au wajinga. Hawafahamu maneno ya kawaida ya malighafi na bidhaa au utaratibu, na kuogopa kuagiza vitu visivyo sahihi. Kwahiyo haikunipasa kufanya kazi kubwa kuirahisisha kwa kila mtu na kwa watu wa aina mbalimbali Watu wengine wanajua vizuri kitu wanachokihitaji wakati huo huo wengine hawana uhakika wanataka nini, au kupanga bajeti ya miradi yao na kwa hakika hupuuzia manufaa na faida ya uwekezaji wao hususan inapokuwa

Biashara ya mabango ya matangazo ni shughuli isiyothaminiwa hata kidogo katika maisha yetu ya kila siku.

Ingawa Tovuti hii imebuniwa kwa shauku kubwa, lakini tunadhani na siyo watembeleaji wote watapitia kwa undani kwenye kila sehemu ya tovuti hii. Na kama wewe ni mmoja wao mazoea ya kurukaruka kurasa, basi usishangae kama haitokutokea hapa kwasababu wakati wa kuandaa tovuti hii, tulikuwa tumetafakari mambo mengi ya kuwavutia watembeleaji kama wewe ili uweze kuperuzi kwa udadisi na kuthamini maelezo ya kina ambayo yamebuniwa kwa watembeleaji wapya, watu mmoja mmoja, wanafunzi, wachoraji wa picha, wenye ujuzi na wasio na ujuzi, wamiliki wa biashara, mameneja wa bidhaa mbalimbali, makampuni ya utangazaji, wabunifu wa mapambo ya ndani, wasanifu majengo, makandarasi pamoja na wajengaji wa majumba, mameneja masoko na ununuzi na hata wakongwe katika tasnia hii. Chukua muda wako adhimu kupitia vitufe vya rangi kama tulivyo viunganisha kuwa rahisi kwako.

Ili kuifanya kuwa rahisi na hata kusisimua Zaidi, mimi binafsi nimeandika makala ambazo utaziona sehemu ya maandiko mtandaoni na maelezo kwenye tovuti hii. (Sehemu ya e-literature & info)

Makala hizi mara kwa mara hupitiwa upya na huwekwa taarifa mpya kwa hiyo usicheze mbali mara tu utakapozisoma ingawaje tutathamini ukweli kwamba umekuwa mtembeleaji wa mara kwa mara, mara nyingine ukitembelea utakuta mambo zaidi ya yale uliyoyaona mwanzoni.

Kama hii ni mara yako ya kwanza kutembelea hapa na umeingia ghafla bila kutarajia, utajisikia kama mtoto mdogo kwenye duka kubwa la pipi na ni mwenye bahati kugundua tovuti hii lakini ambapo hata kama umeitembelea kwa kujua kwa hakika utajisikia kama umeingia kwenye mgodi wa dhahabu wa maelezo na tunatarajia kukuona tena.

Hivyo basi tunaamini kwamba utashawishika kututembelea mara nyingi zaidi. Zaidi ya hayo, pia usisite kutembelea tovuti yetu kwa kununua bidhaa au kuapata huduma zetu, kukutana nasi au kupata ushauri wetu, kuhusu mabango, kujifunza kitu bila malipo/bure, kupata taarifa au kuperuzi kwenye tovuti yetu. Karibu sana.

Pamoja na kuwa mshauri niliyebobea kwenye mabango ya matangazo na alama za biashara, mchoraji picha kwenye kompyuta (Graphic Designer), na mkurugenzi mtendaji wa kampuni yangu, nina mambo tofauti ninayopendelea kuyafanya ndani na nje, mimi ni mwandishi na mtunzi wa mashairi yenye vina, kwa lugha nyepesi yenye misingi ya Imani ya kidini lakini kwa ajili ya usomaji wa kiulimwengu na mada chache za masuala ya kimapenzi pia.

Kwahiyo njoo tuperuzi bila kujikweza 😊

Karibu sana
M. P. Esmail
CEO – Sign Industries Ltd.

Our success is not only because of our internal team work; we also enjoy the teamwork with our clients that adds to the overall experience.